Monthly Archives: F Y

Ndoto na malengo, tofauti yake ni nini?

Ndoto na malengo, tofauti yake ni nini? Mara nyingi sana, mambo haya mawili yamekuwa yanachanganya sana. Je, Ndoto ni sawa na malengo?  Malengo ni sawa na ndoto? Ngoja tuone: Nimesikia mara nyingi sana ‘nina ndoto’ mtetezi wa haki za binadamu Martin Luther King alisema. Mtu anawezaje kulinganisha/ kuhusisha  ‘ndoto’ na ‘malengo’  katika taaluma yangu nimegundua ndoto ni mawazo na malengo ni msingi imara zaidi. Kwa nini ninalisema hili? Ni ngumu kuishikilia/kuing’ang’ani ndoto wakati malengo yanaweza kung’ang’aniwa kutendeka Ninaweza kuwa ninakosea kwa kugawanya mambo haya mawili Continue reading →

Leo ni siku myhimu sana

Leo ni siku muhimu sana Leo ni mwanzo. Ni siku ambayo ninawakaribisha katika ulimwengu wangu wa maono na mitazamo. Ni mwanzo wa maisha yetu yajayo. Hivyo basi, Tunaanzia wapi? Maendeleo? Ndio! Kama tunataka kuleta  maendeleo, kitu ambacho ni lengo kuu la ukurasa huu, yote yataanza kwa ‘UTAYARI’. Kama UTAYARI upo, hatua inayofuata ni MABADILIKO! ndio, amini usiamini, maendeleo yanahitaji mabadiliko na ni ubunifu wa mabadiliko ambao ninaenda kuuzungumzia hapa kati ya vitu vingine. Sote tunahitaji kuendelea, lakini sio mara zote au sio mara zote tumejiandaa Continue reading →